'Sikufikiria kuna wanaume wa kweli wanaomsaidia mwanamke -Tanasha Donna

Aliyekuwa mwanahabari wa redio ya NRG Tanasha Donna, alinena na kusema kuwa hakujua kama kuna wanaume ambao wangesaidia mwanamke bila ya kutarajia chochote kutoka kwao.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii, Tanasha alisema kuwa hakufikiria mtu yeyote hangefanya chochote bila ya kumjaribu.

Tanasha alimsifu mwanahabari wa runinga ya KTN Jamal Gaddafi na kusema kuwa amemuonyesha msaada wa kweli ambao hangetarajia mwanamume yeyote kumfanyia na bila hata kujisifu hadharani.

"Siku zilizopita sikufikiria kama kuna mwanaume ambaye angesaidia mwanamke kwa ukweli bila hata kutarajia kitu kutoka kwake bila ya hata kufanya chochote na mimi kama mwanamke.

Bila hata kujisifu kwenye mitandao na hadharani ni msaada tu wa ukweli. Asante  ❤️🙏🏽❤️." Aliandika Tanasha.

Maneno yake yanakuja siku chache baada ya kueleza uhusiano ambao upo kati yake na mwanahabari huyo.

Kulingana na mama huyo wa mtoto mmoja alisema kuwa Gaddafi ni miongoni mwa watu ambao wamemsaidia  kukamilisha na kuendelea na miradi yake.

Aliongeza na kusema kuwa Gaddafi ni kama ndugu yake na anampa heshima inayostahili.

“Jamal is in my team, I have a very small team and we are all very hard working. Jamal is also helping manage a few of my things. We are just one team with one dream. Jamal is my brother, I know his sister and he has a very beautiful wife and a beautiful child has well, and I respect them fully. Jamal is just my brother, he is my family na hata mwenyewe aliulizwa hilo swali and he made it clear that we are just a team and we are very professional but always watu watatafuta something to say, out of anything."Alieleza.