Kifo cha George Floyd: Tunafahamu nini kuhusu maafisa 4 wa polisi waliohusika?

Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi binafsi wa maiti, hatua ya Chauvin ilichangia kifo cha wiki iliyopita cha Mmarekani mweusi George Floyd, ambacho kilisababisha maandamano makubwa nchini Marekani.

Katika video hiyo iliozua ghadhabu, Chauvin- afisa mzungu wa polisi, anaonekana akimzuilia chini Floyd akitumia goti lake kwenye shingo, huku Floyd akilalamika kuwa hawezi kupumua.

Lakini Chauvin, ambaye tayari amefutwa kazi kwa kutekeleza mauaji bila kukusudia, hakuwa peke yake.

Soma pia;

Alikuwa ameandamana na maafisa wenzake Thomas Lane, JA Kueng na Tou Thoa , ambao walishuhudia kukamatwa kwa Floyd bila kuingilia kati hali iliyosababisha kifo chake .

Maafisa wote wanne wanahudumia kitengo cha polisi cha Minneapolis (MPD).

Baada ya video ya tukio hilo baada ya kanda ya video kutolewa, Mkuu wa MPD, Medaria Arredondo, aliwafuta kazi.

Ijumaa wiki iliyopita, Chauvin alikamatwa na kushitakiwa kwa mauaji bila ya kukusudia.

Lakini maafisa watatu waliosalia walifanywa nini?

Sababu ya maandamano

Baada ya kufungwa pingu, bwana Floyd alikubali kushikwa huku bwana Lane akielezea alikuwa anakamatwa kwa kutoa pesa bandia.

Ni wakati maafisa wa polisi walipojaribu kumuingiza bwana Floyd katika gari lao ndiposa mvutano ukatokea.

Baada ya mvutano kidogo wa kujaribu kumuingiza Floyd ndani ya moja ya magari ya polisi, Chauvin alimzuilia chini uso huku uso wa mwanamume huyo ukiwa umebamizwa sakafuni, nae Lane akishikilia miguu yake na Kueng akizuilia chini sehemu ya mgongo.

Thao alikuwa amesimama kando ya gari hilo.

Tunachokifahamu kuwahusu maafisa hao

. Hakuna maelezo ya kina kuwahusu maafisa hawa.

. Tou Thao aliwahi kushitakiwa mwaka 2017 kwa madai ya utumizi wa nguvu kupita kiasi.

. Kesi hiyo ilikamilishwa baada ya kuamuliwa. Malalamishi mengine sita yaliripotiwa dhidi ya Thao.

. Tano kati ya kesi hizo zinaendelea. Rekodi zilizotolewa kwa umma hazina maelezo zaidi kuhusiana na kesi hizo.

. Thomas Lane alijiunga na MDP mwaka 2019. Hakuna rekodi yoyote ya mashitaka dhidi yake.

. Hakuna taarifa kuhusu historia ya kikazi ya J. Alexander Kueng. Pia hakuna rekodi yoyote ya mashitaka dhidi yake.