Mamake Abenny Jachiga alazimika kukalia kaburi ili kuzuiya kundi la vijana kufukua mwili

ABENNY-JACHIGAS-MUM
ABENNY-JACHIGAS-MUM
Mama wa mwanamziki mwenda Abenny Jachiga,Monica Auma asubuhi ya leo amelazimika kukalia kaburi la mwanawe ili kuzuiya halaiki ya vijana waliokuwa wamewasili nyumbani kwake kufukua mwili wa msanii huyo baada ya kuzikwa usiku wa kuamkia hii leo.

Vijana hao wanaripotiwa kukashifu hatua ya kuzikwa kwa Abenny usiku wakisema kuwa jamii ya Wajaluo inaruhusu tu mtu aliyejinyonga kuzikwa usiku .

“Jachiga did not commit suicide, he died after a short illness. We want to exhume his body and give him a decent send-off that befits his stature,” mmoja wa vijana hao amenukuliwa.

Jaribio lao lilitibuliwa baada ya mjane wa mwendazake na mamamkwe kukalia kaburi.

“You want to kill me! Don’t exhume my son’s body,” Auma alifoka.

Jachiga anaripotiwa kufariki kutokana na nimonia alhamisi mwezi huu tarehe 11.