Tanasha Donna amsherehekea Diamond siku ya kina baba Ulimwenguni

Japo waliachana kwa muda, Msanii wa humu nchini Tanasha Donna alichukua muda wake kumsherehekea baba wa mwanawe Diamond wakati ulimwengu ulikuwa unaadhimisha siku ya akina baba.

Akifuata mtindo huo, Hamisa Mobetto ambaye amejaaliwa mtoto na Diamond, alimtakia heri njema katika maadhimisho hayo kama baba wa mwanawe.

"Happy Father's Day to you father Dee. May God protect and make everything easier without forgetting to always have fun. I and @deedaylan love you very much @diamondplatnumz," Hamisa

Zari pia hakusahaulika katika usanjari huo kwani alitumia muda wake kumtakia kila la heri Diamond maishani.

"Happy Father's Day baba four, pray for life to see them grow into great adult beings (it's every parent's wish) glad to see you doing your part now. We appreciate you," Zari

Hiyo jana wapenzi tofauti walitumia muda wao kuwatakia kila la heri wazazi wa jinsia ya kiume kote ulimwenguni.