Watu 149 wamepatikana na virusi vya corona

EbcFi_VXsAAFj-Y.jfif
EbcFi_VXsAAFj-Y.jfif
Katika taarifa ya kila siku na iliyotumwa kwa vyombo vya habari nchini ,Kenya imesajili visa 149 vya maambukizi ya corona baada ya watu 3090 kufanyiwa vipimo ,hivyo,kufikisha wagonjwa 5533 wa virusi hivyo nchini.

Vile vile taarifa hiyo imesama kuwa watu wengine 48 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha jumla ya watu 1905 waliopona.

Aidha wagonjwa 5 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo ,na kufikisha watu 137 waliofariki.

Visa hivyo vipya vimetokea maeneo yafuatayo,Nairobi (73), Mombasa (20), Kiambu (8), Machakos (3)

Kati ya waathiriwa hao ,wakenya ni 148 huku raia wa kigeni akiwa mmoja.

Wakati uo huo taarifa hiyo imeonya kuwa watu wanaotumia chang'aa wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

Waathiriwa ni kati ya mwaka mmoja na 76.