Watu 120 zaidi wapatikana na virusi vya corona- Rashid Aman

Watu 120 zaidi wamepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 na kufanya taifa la Kenya kusajili idadi ya jumla ya watu  6190 walioathiriwa na virusi hivyo.

Watu hao wamepatikana baada ya sampuli za watu 2,221 kufanyiwa vipimo.

Wakati huo huo watu 42 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha watu 2,014 waliopona virusi vya corona.

Aidha mgonjwa mmoja amefariki na kufikisha watu 144 waliopoteza maisha kutokana na virusi hivyo hatari.

Kati ya visa hivyo vipya, Wanaume ni 86 huku wanawake wakiwa 36.

Nairobi imesajili visa 67 kati ya visa hivyo vipya huku kaunti ya Mombasa ikisajili visa 17.

Kufikia sasa tangu kuripotiwa kwa virusi hivyo nchini, kaunti zifuatazo ndizo zilizosajili idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi hivyo, Nairobi 3031, Mombasa 1445, Busia 407, Kajiado 242 na Kiambu 222.

MHARIRI; DAVIS OJIAMBO