Kibaki hayupo Hospitalini –Msaidizi

Rais mstaafu Mwai Kibaki hayupo hospitalini .katibu wake wa kibinafsi  Ngari Gituku  amesema ingawaje ni kweli kwamba kibaki alikuwa hospitali maajuzi ,ilikuwa ni uangalizi wa kawaida na hajalazwa .

Gituku ametaja kama  ‘kuongezwa chumvi’ kwa ripoti katika vyombo vya habari kwamba Kibaki amekuwa hospitalini kwa siku kumi . Amesema Kibaki alitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani .

Msaidizi huyo wa Kibaki amesema   hapafai kuwa na  hofu wakatu mtu mashuhuri anapopelekwa hospitalini  kwani ni jambo la kawaida kufanyiwa uangalizi wa kila mara .

Kibaki amekuwa na tatizo la goti tangu alipohusika katika ajali ya barabarani mwaka wa 2002  huo Machakos akifanya kampeini . Amekuwa akifanyia uangalizi na matibabu ya goti hilo tangia wakati huo .