Mama mwenye uvimbe usoni kulipiwa upasuaji na gavana Ngilu

Gavana wa Kitui Charity Ngilu ameahidi kugharamia upasuaji wa mama mmoja raia wa Tanzania aliye na uvimbe kidevuni.

Kupitia ujumbe kwenye twitter siku ya Alhamisi  jioni, Ngilu alifichua kwamba alikutana na mama huyo, Pendo Masonga mwenye umri wa miaka 20 katika kaunti ya Nairobi.

Soma pia;

Alipoona uvumbe kwenye uso wake alizungumza naye na mwanamke huyo akamwambia kwamba alikuwa ameishi na hali hiyo kwa muda mrefu.

Masonga, ambaye ana mtoto mdogo inasemekana alihamia nchini Kenya kwa lengo la kukutana na wahisani  kumsaidia afanyiwe upasuaji kurekebisha uvumbi usoni mwake.

Soma pia;

"Nimejitolea kulipia matibabu yake katika Hospitali ya Rufaa ya Kitui. Mgonjwa huyo tayari amechukuliwa kupelekwa katika Hospitali ya rufaa ya Kitui," Ngilu alisema.

Mwaka 2018 Ngilu alifungua hospitali ya kisasa ya rufaa katika kaunti ya Kitui kwa lengo la kuimarisha huduma za afya katika kaunti hiyo. Hospitali hiyo imerahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakaazi wa kaunti hiyo.

Soma pia;

Mwaka huo huo mtaalam wa upasuaji wa usoni Daktari Arelis Rabelo Castillo kutoka Cuba alitekeleza upasuaji wa kwanza kama huo katika kaunti ya Kitui.