Ndoa sio kalongolongo: Kabla ya kuoa ama kuolewa ni yepi unayofaa kujua? Matarajio yako yanafaa kuwa yepi?

kalongo (1)
kalongo (1)
Watu wengi hujiingiza katika ndoa bila kujua wanajiingiza katika suala lipi na kama ilivyodhihrika wiki iliyopita, wengi hujitosa katika ndoa wakiwa na matarajio mbalimbali ambayo baadaye huwafelisha. Msanii wa Tanzania Shilole aligonga vichwa vywa habari kwa kuibuka na madai kwamba mumewe Uchebe alikuwa akimpiga na amekuwa katika ndoa ya Dhuluma.  Kwa mengi zaidi kuhusu sakata ya shilole basi isikize podi hii yenye maelezo ya kilichomfanyikia

&t=101s

Naye msanii wa Gospel wa Kenya Betty Bayo alizuka na mapya akisema hakufanya harusi kabla ya kuanza kuishi na mhubiri  Kanyari. Kanyari  na Bayo amekuwa kaiweka jumbe za kupigana vijembe kuhusu ndoa yao iliyofeli huku kila mmoja akionekana kujutia alichofanya kwa kujiingiza katika uhusiano na mwenzake.

 Sikiza  Podi hii ufahamu unayofaa kujua kabla ya kujitosa katika ndoa .

&t=278s

Kwa upande wa Shilole, aliweka kwenye instagram msururu wa picha zinazoonyesha siku tofauti tofauti ambazo amekuwa akipigwa na mumewe na pia kuomba radhi kwa  kuishi ni kana kwamba kila jambo katika ndoa yake limekuwa shwari. Amesema ameamua kuvunja kimya hicho ili wanawake wengine wapate ujasiri wa kusema wanayopitia.

Aliandika

Naandika haya, nikiwa na akili timamu na utulivu, La kwanza kabisa nataka KUOMBA RADHI JAMII YANGU. Naomba radhi kwa sababu niliwaaminisha ndoa yangu haina tatizo, huku ukweli ukiwa hauko hivyo, nimekuwa mtu wa kuambulia vipigo na MENGINE yasiyozungumzika, Naomba radhi kwa sababu niliposikia wanawake wenzangu wakipigwa niliwaambia PAZENI SAUTI, niliposikia mwanamke kule Kigamboni ameuwawa na kuchomwa moto niliomboleza na jamii na kusema Bora angesema”.. huku mimi nikijikausha na kujitoa kwenye kundi lao wakati ukweli wangu MIMI NI MWENZAO, Naomba radhi.

Mimi ni kioo cha jamii, tena sura kubwa ya wanawake. Leo numeona nivunje ukimya kwa kuweka wazi kwamba MUME WANGU ASHRAFU SADIKI, maarufu kama UCHEBE AMEKUWA ANANIPIGA SAAANA, na tena hata baada ya kunipiga hajali kupiga simu wala kujua naendeleaje, nauguzwa na watu baki hospitali, na bado manyanyaso mengine yanayoikosesha hii ninayoiita Ndoa uhai na furaha

na zaidi nina WATOTO, watoto wanaoniangalia kama Baba na Mama, leo nikubali kufa na kuacha wanangu barabarani, SITAWEZA

.

‘Uchebe’ ni mwanaume niliyempenda, nilimvumilia kwa madhaifu yote, nikampa kila kitu, (Utu wangu, Mali Zangu na hata palipotakiwa kumuendeleza asimame mwenyewe nilifanya kwakuwa nilijua tuko pamoja), lakini HILO HALIKUWAHI KUZUIA VIPIGO, DHARAU NA USALITI.

.

Siku 2 zilizopita baada ya kutoka SABASABA KUTAFUTIA WATOTO WANGU NA KUMTAFUTIA YEYE NILIPIGWA SANA. SABABU ZA KUPIGWA NI MIGOGORO MIDOGO YA KAWAIDA AMBAYO IPO KWENYE KILA NDOA, sio kwamba amenifumania au mambo yanayoshindwa kuzungumzika, hapana, Tena Namuheshimu sana, lakini solution aliyoiona ni kunipiga kinyama bila huruma, tena kwa kunishtua na ngumi nikiwa usingizini, Kama mnavyoona picha hapo ni matukio ya siku tofauti tofauti.