Hofu baada ya mlinzi mmoja wa Gavana Joho kupatikana na virusi vya corona

Joho
Joho
Mlinzi mmoja anayemhudumia gavana wa Mombasa Hassan Joho ameripotiwa kupatikana na  Covid-19.

Mlinzi huyo  ambaye ni miongoni mwa wanne ambao humlinda Joho  alipatikana na virusi hivyo akiwa Nairobi  na wote wamewekwa katika karantini, Mombasa Beach Hotel. Katibu wa kaunti Dennis Maganga Lewa,  alilieleza gazeti la The Star kuzungumza na waziri wa afya  katika kaunti   Hazel Koitaba,  ambaye amesema yuko mkutanoni.

" Mtu bora wa kujibu hilo ni waziri. Tafadhali mpigie’ Lewa amesema

Wakati wa kuichapisha taarifa hii waziri huyo hakuwa ametoa jibu kuhusu ripoti hizo . Duru zaarifu kuwa  mlinzi huyo alikuwa na gavana kwenda Nairobi kwa vikao  vya senate na alipatikana na ugonjwa huo  baada ya vikao  hivyo ,siku chache kabla ya Joho kusafiri nje ya nchi .

Wote walipelekwa kwa ndege hadi Mombasa  na iliainika kwamba hakuwa na daalili wala hali yake haikuwa mbaya ili kulazimu lazwe hospitalini . Gavana Joho na wafanyikazi wake wa karibu hufanyiwa vipimo vya kila mara kila baada ya wiki mbili .

" Wakati huo walikuwa wamekwenda kwa vipimo hivyo ,Joho hapendi kujitia hatarini  .kwa sababu unajaua wanatangamana na watu wengi’ duru zimearifu . Mombasa ni kaunti ya pili kwa kuwa na visa vingo vya wagonjwa wa Covi 19 baada ya Mombasa . kufikia jumatatu Mombasa ilikuwa na visa  1, 726 .  Mkuu wa wafanyikazi katika afisi ya Joho Joab Tumbo hata hivyo amesema hajajulishwa kuhusu kisa hicho .