ovid-19: Kenya yasajili visa 603 vipya vya virusi vya Corona

Wizara ya afya imetangaza visa 603 vipya vya virusi vya Corona.

Hii ni baada ya sampuli 5724 kufanyiwa vipimo huku idadi ya walioambukizwa ikifika 13,353.

Hayo yakijiri, wagonjwa 682 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Idadi ya waliopona sasa imefikia 5122.

Watu tisa wameaga dunia na kufikisha 234 idadi ya watu waliofariki kufuatia virusi hivyo vya corona, humu nchini.

Kufikia sasa, watu 243, 887 wamepimwa virusi hivyo vya corona.