Ni mara ya nne kwa spika kuahirisha mjadala kuhusu suala hilo baada ya kundi aliloliteua kupata mwafaka kukosa kukubaliana .
Kila kambi imekuwa na msimamo mkali na kuzuia uwezekano wa kuafikia mfumo wa pamoja unaoweza kutumiwa kugawa raslimali kwa kaunti kwani wale ambao kaunti zao zingepata mgao wa juu wameutetea vikali mfumo mpya ilhali wale kutoka kaunti zilizotengwa wanataka hali ya sasa isalie .
Chini ya mfumo uliopendekezwa kaunti za Garissa, Wajir, Marsabit, Isiolo, Samburu, Turkana, Tana River, West Pokot, Lamu na Mandera zitapokea jumla ya shilingi bilioniu 17 .
Wajir itapoteza shilingi bilioni 2 billion, Marsabit na Mandera bilioni 1.9 kila moja ilhali Garissa itasalimisha shilingi bilioni 1.6 billion nayo Tana River itapoteza Sh1.5 billion.
Uasin Gishu, Nakuru, Kiambu, Nandi na Kakamega c zitapata mgao wa juu .