Nimechoka siku moja Mungu atafichua ukweli-Terence Creative azungumzia kutowaona wanawe

Mcheshi Terence Creative amezungumzia uchungu alio nao kwa kutoa waona wanawe kwa muda wa miaka sita, hii ni baada ya kumjibu shabiki moja aliyeuliza mke wake Milly Chebby kama ndiye chanzo cha Terence kutowaona wanawe.

Cheche za maeneno zilianza pale mkewe alijibu swali hilo na kusema kuwa hajui kwa maana alikuwa anaendelea na maisha yake.

"Haki sijui it’s more of moving on." Milly Chebby alijibu.

Shabiki aliyefahamika kama Fabulously Chic alimkosoa vikali Chebby kwa kujibu swahi kiholela ilhali watoto wanahusika katika uhusiano wao.

Pia aliongeza na kusema alichukulia jambo hilo rahisi sana kwa kujibu swali hilo.

"Ni zaidi ya kuendelea na maisha? kawaida?wow!!! unasema haya ilhali watotot wanahusika, watoto wenye wanakua? umechukulia rahisi hivi aki, lakini unachukulia rahisi hivo mpaka pale utajipata katika hali hiyo

Kukimbia hapa na pale juu chini ili kupata msaada." Alisema Shabiki huyo.

Terence ambaye aliona maoni ya shabiki huyo alisema kuwa alikatazwa kuwaona wanawe kwa muda wa miaka sita kwa sababu tofauti na hamna mtu yeyote ambaye anafahamu uchungu ulio ndani yake.

Aliongeza na kusema kuwa kwa maana wamekimya haiwezi maanisha kuwa mambo yote yako sawa.

"@fabulously_chic hufahamu uchungu ulio ndani yagu kwa kuto waona wanangu kwa miaka sita,kwa sababu za ubinafsi ukweli ni kuwa kw amaana tumenyamza haiwezi maanisha kila kitu kikosawa  

Siku moja Mungu atafiichua ukweli wote kwa maana nami pia nimechoka." Aliandika Terence.