Harmonize amsajili msanii wa Nigeria Skales kwenye lebo yake

Msanii wa bongo na bosi wa lebo ya konde music worldwide amemsajili msanii na rappa wa nchi ya Nigeria Skales kwenye lebo yake, wawili hao walitangaza haya kwenye mitandao ya kijamii, huku Harmonize akimkaribisha kwenye lebo hiyo na kuandika,

"Muziki wa Afrika waota kuenda dunia nzima tunafuraha kumkaribisha msanii kutoka Nigeria kaka yangu @youngskales karibu kwa familia@Kondegang ni tumu yenye maono na ndoto 💪 ." Aliandika Harmonize.

Kupitia kwenye posti nyingine Skales ambaye anafahamika sana kwa kibao cha 'fire waist' akimshirikisha Harmonize alisema kuwa lebo ya Konde ndio meneja yake kuanzia sasa na yeyote anataka kushiriki wimbo na yeye anapaswa kuulize maneja ya lebo hiyo.

"Hello wapenzi wangu wa Afrika mashariki, nimesajiliwa kwenye lebo ya konde kirasmi, timu ya @kondegang itasimama nami na kama meneja yangu katika Afrika mashariki LET'S GO!!! 🌍🇹🇿🇳🇬." Aliandika Skales.

Skales ndiye msanii wa pili kusajiliwa na lebo hiyo baada ya msanii wa Tanzania Ibraah kusajiliwa, Harmonize na Skales wameshirikiana kwa nyimbo kadhaa kwa hivyo kufanya kazi pamoja haitokuwa ngumu.