'Akufaaye kwa dhiki....'Vile mcheshi Njugush amesaidia familia ya Abel Mutua kwa miaka,2,

Muigizaji Abel Mutua ambaye alifahamika sana kupitia katika kipindi cha Tahidi high alimshukuru mcheshi Njugush kwa kumsaidia na hata kusaidia familia yake kwa miaka miwili.

Si marafiki wote kwa hakika wanaweza saidia rafikiye kwa muda huo wote.

Kwa ajili ya matendo yake mema ya kumsaidia Njugush wakati alipokuwa anachipuka katika tasnia ya usanii, Abel alimsaidia Njugush kupata ukaguzi wa ucheshi mwaka wa 2013.

Huku akizungumza kupitia youtube alisema kuwa Njugush ni mcheshi mwenye roho njema.

Abel pia alimpa Njugush uigizaji katika kipindi ha te realhouhelps of kawangware, uigizaji mabao ulitamba nchini kote.

" Alipojiunga na kipindi hicho, tulipata mashabiki wengi na hata watu wakaanza kutujua kuliko awali, huku mwka huo ukiisha alifahamika sana na nikamuahidi kuwa nitaakikisha atakuwa mtu maarufu."

Baada ya kufahamika alianza ucheshi wake kupitia kwenye mitandao ya kijamii huku ucheshi wake ukitamba na kuenea sana na kupendwa na wengi.

Mwaka wa 2017 Njugush alipata kazi kubwa huku akimpigia Abel ili kumfahamisha habari hizo njema.

"Aliniambia kuwa kuna mteja amemlipa zaidi ya millioni kwa mkataba wa miezi miwili, wakati huu Njugush alikuwa tayari anapata mshahara wa 200,000 kwa mwezi."

Baada ya muda Njugush alimuandika mkewe Abel Mutua Judy Nyawira kama meneja wa fedha.

Kwa uchesi Abel alieleza jinsi ke wake alikuwa anapata mshahara wa juu,

"Kwa msingi Njugush amekuwa akilisha na kunilisha kwa kiaka miwili sasa , bado nashangazwa na jinsi mambo yalitendeka." Alizungumza Abel.