Soma walichokuwa wanataka kufanya Tanasha Donna na Kevin Omwenga kabla ya kifo chake

Mwendazake mwanabiashara Kevin Omwenga alifahamika sana kupitia kwenye mitandao ya kijamii na hata na watu tofauti kwenye tasnia ya usanii.

Omwenga aliuawa Jumamosi iliyopita baada ya kupigwa risasi kifuani mwake.

Washukiwa wakuu wa mauaji hayo Chris Obure na Robert Ouko wamo mikononi mwa polisi huku uchunguzi ukizidi kufanyika, kablla ya kifo chake Omwenga alikuwa amenunua gari mbili moja ikiwa ni ya aina ya Porsche Panamera inayo nunuliwa kwa millioni 14.

Meneja wake msanii na mtangazaji Tanasha Donna, Castro amesema kuwa mwendazake alikuwa anataka kufanya kazi na Tansha kabla ya kukumbana na mauti yake.

"Mungu pekee ndiye anajua natamani ungefuata njia ambayo ulikuwa umepanga na Tanasha Donna kuwa mmoja wa hudam ya jamii ya Tanasha

Labda ungekuwa hai sasa G wangu lakini Mungu anajua bora lala salama Kev almaarufu Rich Man."Meneja wa Tanasha Aliandika.

Kulingana na upasuaji Omwenga alipigwa risasi kwa makusudi na wala si bahati mbaya wala ajali kama vile alivyodai Ouko.