Waliachana! Naisenya mbona aliacha na muigizaji wa Maria Luwi

Mwanamke mmoja wa kenya anayeihsi ng’ambo kwa jina  Jacque Naisenya aliyekuwa katika mahusiani na muigizaji wa Brian Ogana aka Luwi  amefichua kwamba hawapa katika uhusiano .

Akijibu maswali ya mashabiki wake mtandaoni   mwanadada huyo alisema hana tena uhusiano na Luwi.

Luwi  alikuwa katika  jarida la mwezi huu la Parents na wanawe watatu hatua iliyowashangaza wengi kwani palikuwa na uvumi kwamba Naisenya ndiye aliyekuwa mama ya watoto wake . Lakini mwanadada huyo alijitokeza kusema

 tafadhali mniruhusu  kubaini hili  sina mtoto na yeyote  natumai hilo sasa lipo dhahiri  na linajibu maswali yenu

 

Miezi michache iliyopita  Brian Ogana alifichuliwa na  mwanamke mmoja kwa kujaribu kumlaghai pesa . Luwi hata hivyo aliyakana madai hayo  akisema ilikuwa njama ya kumharibia jina  .