‘Nitampost vipi mume wa mtu?’ Joyce Maina ajibu madai kwamba yupo katika uhusiano wa pembeni na DJ Mo

Mtangazaji wa Runinga Joyce  Maina amejitokeza kukanusha vikali kwamba  analenga kuvuruga nyumba ya  Size 8 na Dj Mo baada ya kuzuka madai kwamba picha ya mwanamme aliyekuwa naye ilikuwa ya DJ Mo –mume wake msanii Size 8

Muimbaji huyo na Dj Mo hata hivyo wamesalia kimya kuhusu sakata hiyo  na kumekuwa na uvumi kwamba wamekuwa wakipitia matatizo ya ndani ya ndoa kwa miaka kadhaa sasa .

Uvumi huo ulizidishwa na hatua ya Sze 8 kutomfuata mumewe katika instagram . DJ Mo ametajwa kuwa mwanamme aliyekuwa amempakata kimapenzi Joyce Maina katika picha iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii.

Joyce Maina  amejitokeza kukakana madai hayo akiandika;

 “ Habari feki zina vichekesho ,weh.kwa hivyo watu walikosa kumjua mwanamme huyo (mna picha isioonekana voizuri  na inayoonyesha tu kivuli) na sasa kwa ghafla  mtu huyo ni DJ Mo.lol ninyi watu mgenpata A+ katika insha  kuandika  juu hi story mmejiandikia.”

Aliongeza kwamba yeye sio  mjinga kuiweka picha ya mume wa mtu mtandaoni