Washirika wa Ruto wamtaka rais Uhuru kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi

Wabunge wa Jubilee wanaomuunga mkono naibu wa rais William Ruto sasa wanamtaka rais Uhuru Kenyatta  kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi  kwa  ajili ya kutotekelezwa kwa kanuni ya usawa wa kijisnai kama alivyoshauri  jaji mkuu David Maraga.

Wabunge  hao wamesema rais  anafaa kutekeleza  matakwa ya katiba aliyoapa kufuata  kwa kulivunja bunge  ili kuwezesha uchaguzi kuandaliwa . wamesema pia kwamba wako tayari kuzitetea nafasi zao

Miongoni mwa wabunge waliotoa wito huo kwa rais ni mbunge wa Kuria magharibi  Mathias Robi ,Charles Gimose  wa Hamisi  miongoni mwa wengine wakati walipokuwa wakiwahutubia wananchi katika eneo bunge la Bumula  ,huko Bungoma .

Mbunge wa Gatudu Kusini Moses Kuria aliwashauri kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na Moses Wetangula wa Ford Kenya  kukoma kuwapeleka wakenya katika upinzani.

Amesema  mrengo unaomuunga mkono Ruto utaunda serikali  ijayo na  hataki watu wa eneo la magharibi kujipata katika upande wa upinzani .

Mbunge Gachagua Nderitu wa Mathira  alimshambulia  katibu mkuu wa muungano  wa COTU Francis  Atwoli akisema kwamba Atwoli haiwakilishi jamii ya Waluhya .