'Katika uhusiano msiweke kiwango ambacho si halisi,' Size 8 Azungumzia haya

Msanii Size 8 akiwa katika kipindi chao alifichua kwanini hakuweza kuwa na harusi kama vile wengi walitarajia wataweza kutazama harusi ya kifahari ya mwanamuziki huyo.

Huku akipeana sababu kwanini hayo yote hayakutendeka Size 8 alikuwa na haya ya kueleza wakati wa kipindi cha Dine With the Muraya's'

"Wakti Mo na mimi tuliamua kufunga ndoa alikuja kwetu na kukutana na wazazi kwa ajili ya mipangilio,tulipatana na muhubiri na tukaombewa

Wazo hilo ni mimi nilikuja nalo na si DJ Mo, tumekuwa kwa miaka,7, kitu ambacho nimegundua ni kuwa mambo ambayo nilikuwa na yaona nikiwa sijaingia katika ndoa sasa nayaona tofauti

Harusi ni nzuri lakini watu wengi hufanya harusi na kuachwa na madeni kwa maana huchukua mikopo ili kufanya harusi za kifahari

Sababu kubwa kwanini watu hupeana talaka ni kwa ajili ya pesa, kwa hivyo ni afadhali kufanya kitu rahisi na nafuu katika uhusiano hampaswi kuweka kiwango ambacho si rahisi

Wekeni kiwango ambacho mnaweza kudumisha."Alizungumza Size 8.

Ndoa ya wawili hao ni ya kupigiwa mfano na kutamanika na wengi licha ya changamoto za ndoa.