'Demokrasia na nguvu za watu zimeshinda,'DP Ruto ampongeza Feisal Bader

Muhtasari
  • DP William Ruto ampongeza Feisal Bader kwa ushindi wake, na pia amewashuuru watu wa Msambweni

Naibu William Ruto kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter amempongeza Feisal Bader kwa ushindi wake wa kiti cha ubunge katika eneo la Msambweni.

Feisal, ambaye alikuwa anaungwa mkono na Naibu Rais William Ruto alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo mdogo baada ya kujizolea kura 15, 251 dhidi ya 10, 444 za mpinzani wake wa chama cha ODM Omari Boga.

Katika uchaguzi huo mdogo wengi waliamini kuwa mwanaiaji kiti hicho wa chama cha ODM ataibuka mshindi.

 

Katiu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna alikubali matokea na hata kumpongeza mshindi Bader.

"Pongezi sana rafiki yangu Feisal Bader, Ushindi wako unakumbuka imani yetu kwa Mungu na watu,demokrasia na nguvu za watu zimeshinda

Watu wa Msambweni Mungu awabariki Pongexi E.Mwihaki(Gaturi), S.Wanango(Lakeview), K.Ochieng( Wendani) na washindi wote,kwa wale wengine wakati wenu Kwa wengine kuna wakati mwingine." Aliandika DP.