Irungu Kang'ata anapaswa kuzawadiwa kwa kuokoa BBI-Gavana Alfred Mutua

Muhtasari
  • Gana Alfred Mutua asema kwamba Kang'ata anapaswa kusifiwa na kuzawadiwa na wala si kulaaniwa kwa barua yake 
  • Pia gavana huyo alimsifia Kang'ata kwa msimamo wake
  • Siku ya Jumatatu Kang'ata alisema kwamba hakupea vyombo vya habari barua aliokuwa amemwandikia rais wala ni mtu mwingine
alfred mutua
alfred mutua

Gavana wa kaunti ya Machakos Alfred Mutua kupitia kwa baadi ya jumbe zake kwenye ukurasa wake wa twitter alisema badala ya kumsuta.

Kulingana na gavana huyo Seneta huyo wa Murang'a aliokoa ripoti ya BBI.

PIa gavana huyo alisema kwamba Kang'ata alizua maswala muhimu kuhusu BBI na badala ya kumlaani kwa kumuandikia Mkuu wa Nchi, wasiwasi wake unapaswa kushughulikiwa.

"Seneta Irungu Kang'ata anapaswa kuheshimiwa na kuzawadiwa kwa kuokoa BBI, barua yake Kang'ata kwa rais Uhuru Kenyatta kwa mtazamo wake wa kuunga mkono rioti ya BBI katika mlima kenya." Aliandika Mutua.

Pia alimpongeza seneta huyo kwa ujasiri wake aliokuwa nao kwa kumwandikia rais Barua.
 
"Kwa hivyo, badala ya kulaani na kutoa shinikizo kwa kiongozi mwenzangu @Irungu Kang'ata sisi ambao tunaunga mkono ripoti ya BBI tunapaswa kumsifu 
 
Naunga mkono BBI na uongozi wake rais Uhuru Kenyatta na miradi na kitu chochote ambacho kinachangia mafanikio yake kimekaribishwa kwangu."
 
Matamshi yake Mutua yanajiri baada ya Kang'ata kusutwa na kukejeliwa na baadhi ya wanasiasa.