Covid-19:Watu 345 wapatikana na corona,143 wapona,4 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 345 wapatikana na corona,143 wapona,4 waaga dunia
  • Wagonjwa 58 wapo katika kitengo cha ICU
Picha: REUTERS
Picha: REUTERS

Visa 345 vya corona vimeripotiwa nchini siku ya Jumatano baada ya sampuli 5,550 kupimwa katika saa 24 zilizopita .

Idadi hiyo inafikisha 106,470 jumla ya visa hivyo hadi sasa huku sampuli zilizopimwa zikifika 1,306,601.

Kutoka visa hivyo 294ni wakenya ilhali raia wa kigeni ni 51 . mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 2ilhali wa umri wa juu ana miaka 93.

Wagonjwa 205 ni wanaume huku 140 wakiwa wanawake, kulingana na kaunti, kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 198 vipya vya maabukizi ya corona ikifuatwa na kaunti ya Kiambu na visa 44.

Wagonjwa 143 wamepona ugonjwa huo huku idadi hiyo ikifika 86,860 Watu 121 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 22 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 4 wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo na kufikisha idadi jumla 1,863ya watu walioga dunia.

Kuna wagonjwa 378 ambao wamelazwa hospitalini ilhali 1,494 wapo chini ya mpango wa utunzi nyumbani .

Wagonjwa 58 wapo katika kitengo cha ICU.