Gladys Wanga akataa kwenda mbele ya NCIC juu ya sherehe ya siku ya wanawake

Muhtasari
  • Gladys Wanga akataa kuenda mbele ya NCIC leo, huku akisema kwamba ni siku ya wanawake duniani
  • Wanga alisema kwamba ataonekana siku nyingine na wala si leo
  • Wanga alisema NCIC inaonekana kurudisha nyuma wakati wa giza kuwaita viongozi wa kisiasa kuficha makosa
Gladys Wanga

Mwakilishi wa wanawake wa Homabay Gladys Wanga amekataa kukutana na NCIC leo juu ya makosa ya uchaguzi akisema anasherehekea Siku ya Wanawake Duniani.

"Kwa sura ya kibinafsi, mialiko hii inaonekana kuwa na chapeo ili kuficha wale waliotenda makosa ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwashambulia maafisa wa IEBC pamoja na wanawake - ambayo nilipinga vikali," alisema.

Katika taarifa Jumatatu, Wanga alisema yuko tayari kuonekana wakati wowote lakini sio leo.

 

"Ili kunisaidia kujiandaa na kujielewa, naomba mashtaka dhidi yangu au maswala unayohitaji kujishughulisha nayo," Wanga Alisema.

Wanga alisema NCIC inaonekana kurudisha nyuma wakati wa giza kuwaita viongozi wa kisiasa kuficha makosa.

Siku ya Ijumaa, Seneta wa Kakamega Cleophas Malala na Wanga na Aisha Jumwa walikuwa miongoni mwa wabunge 10 ambao waliitwa na NCIC kuhojiwa juu ya ghasia zilizotikisa uchaguzi mdogo wa Alhamisi iliyopita nchini kote.

Wengine ni wabunge Faisal Bader (Msambweni), John Waluke (Sirisia), Ben Washiali (Mumias Mashariki), Chris Wamalwa (Kiminini), Charles Were (Kasipul), Fred Kapondi (Mt Elgon) na Seneta Mteule Millicent Omanga.

Mwenyekiti wa NCIC Samuel Kobia Jumamosi alisema wabunge hao wanatarajiwa kufika mbele ya tume hiyo Jumatatu kuangazia majukumu waliyocheza wakati wa machafuko yaliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi siku ya Alhamisi wiki iliyopita.