Soma ujumbe wake rais Uhuru wa kuwatia moyo watahiniwa wa mtihani

Muhtasari
  • Uhuru Kenyatta awatia moyo watahiniwa wa mtihani,huku akiwatakia heri njema wanapokalia mitihani yao
Image: PSC

Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa kutia moyo kwa watahiniwa wa mwaka huu wanapoketi kwa mitihani yao ya kitaifa.

Akiongea wakati wa hotuba yake kwa taifa  Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi, Uhuru aliwaambia watahiniwa wote kwamba licha ya kufanya mitihani baada ya kuwa nje ya darasa kwa karibu mwaka, nchi nzima na yeye mwenyewe wanamini kwamba watafanya vyema katika mitihani yao.

"Kama baba na kama Rais, najua umefika wakati wa kukalia mitihani yenu, baada ya kupitia changamoto ambazo hazijapitiwa na wengi kabla yenu

Kwa watahiniwa wetu wa Darasa la Nne, Darasa la Nane na Kidato cha Nne, ninawasilisha matakwa yangu mema kwa nyinyi wote na ninaomba kwamba juhudi zenu zitazaa mavuno mengi," Uhuru alisema.

Mitihani ya KCPE itaanza Machi 22 na kumalizika Machi 24 kwa watahiniwa 1,187,517.

Watahiniwa wa KCSE watafanya mazoezi yao mnamo Machi 25 kabla ya kufanya mtihani kutoka Machi 26 hadi Aprili 21, ihuku watahiniwa wakiwa 751,150.