Mwanamke akamatwa kwa kuwadhuru watoto wa mwajiri wake

mjakazi aliyewadhulumu watoto
mjakazi aliyewadhulumu watoto

Mwanamke mmoja wa umri wa makamo anayedaiwa kuwadunga kisu watoto wa mwajiri wake wa zamani, alikamatwa jana alipokuwa akijaribu kutoroka.

Mwanamke huyo alifutwa kazi wiki tatu zilizopita na anaaminika aliregea nyumbani kwa mwajiri wake na kuwashambulia watoto hao, wazazi wao walipokuwa hawako.

Alikamatwa mjini Eldoret akiwa kwenye basi kuelekea Busia. DCI amewashukuru wananchi kwa kusambaza picha na video za mwanamke huyo, na kupelekea kukamatwa kwake.

Hizi ni baadhi za habari tunazozipa kipau mbele humu nchini;

Wanafunzi 11 kutoka shule ya wasichana ya Manga Girls katika kaunti ya Nyamira County walijeruhiwa jana walipokuwa wakimuokoa mwenzao aliyejaribu kujitoa uhai kwa kuruka kutoka kwa darasa lililokuwa kwenye ghorofa ya pili.

11 hao walipata majeraha madogo lakini wakaweza kumuokoa mwenzao asijirushe nje. Mwanafunzi huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Sengera, maafisa wakijaribu kutambua chanzo cha kutaka kujitoa uhai.

Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa iliharibiwa jana katika hoteli ya Oasis resort mjini Malindi, kaunti ya Kilifi, baada ya moto kuteketeza hoteli hiyo. Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Malindi John Kemboi anasema moto huo ulichochewa na upepp mkali ulioupelekea kusambaa kwa majengo yaliyokuwa karibu. Chanzo cha moto huo hakujajulikana.

Hatma ya katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion katika uongozi wa muungano huo sasa inayumbayumba baada ya mgombea aliyemtaka kukosa kushinda wadhfa wa tawi la Kericho katika uchaguzi hapo jana. Mpinzani wake Stanley Mutai alipata kura 312, na kumshinda Anne Chepkoech aliyepata kura 294. Mutai ameapa kumbandua Sossion kutoka kwa wadhfa wa katibu mkuu katika uchaguzi ujao, akisema walimu.

Kiongozi wa chama cha Ford-Kenya Moses Wetangula sasa anawataka polisi kuwapa barakoa wananchi badala ya kuwakamata wanaopatikana hawajavalia barakoa. Viongozi wa magharibi pia wanaitaka jamii hio kusali na umoja, uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 unapokaribia, licha ya wagombea kadha kujitokeza.