'Mawakili kuondoka kortini ni mbaya,'Wakili Ahmednasir azungumza baada ya wakili wa Sonko kuondoka mahakamani

Muhtasari
  • Wakili Ahmednasir azungumza baada ya wakili wa Sonko kuondoka mahakamani
  • Siku ya Jumatatu, Ogoti aliamuru Sonko afike kortini kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake ya ufisadi ya shilingi milioni 10 ambayo ingeendelea Jumanne
35f9ec2136abd940 (1)
35f9ec2136abd940 (1)

Siku ya Jumanne drama ilishuhudiwa katika Korti ya Sheria ya Milimani wakati wakili wa Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko John Khaminwa aliondoka kwenye kesi hiyo Jumanne kwa kupinga, akisema hakimu wa kesi hiyo sio sawa.

Akiongea na Wanahabari katika korti za sheria za Milimani, Khaminwa alisema Hakimu Mkuu Douglas Ogoti amekuwa akiamua wazi dhidi ya kezi za Sonko.

Siku ya Jumatatu, Ogoti aliamuru Sonko afike kortini kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake ya ufisadi ya shilingi milioni 10 ambayo ingeendelea Jumanne.

 

Baadhi ya madai kutoka kwa Wakili Khaminwa ni kwamba korti ilizuia haiba ya vyombo vya habari kutoka kwa kesi ya Sonko ikisema kwamba kesi ya Sonko ilikuwa nyeti sana kwa hivyo umma unapaswa kujua kesi hiyo.

Alinukuu hata katiba chini ya kifungu cha 50 ambacho kinatoa haki kwa umma kupata habari.

Ahmednasir ambaye ni wakili mashuhuri Nchini alishutumu mwenendo wa korti ambayo inaweza kuwa ilisababisha Mawakili wa Sonko kutoka nje ya korti na kujiondoa kwenye kesi hiyo.

"Mawakili kuondoka kortini ni mbaya. Kwa daktari Khaminwa kutoka nje ya korti, mwenendo wa korti lazima uwe mbaya sana na wa kutisha hivi kwamba Daktari aliachwa bila njia mbadala

Katika mambo mengi yeye ni sawa ... baada ya yoteamekuwa kortini kwwa miaka mingi," Aliandika Ahmednasir.