Covid-19: 17 waaga dunia,747 wapatikana na corona,114 wapona

Muhtasari
  • Watu 747 wapatiana na corona huku 17 wakiaga dunia
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 120,910kutoka kwa sampuli 1,414,865

Kenya siku ya Jumapili ilisajili visa vipya 747 vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,145 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 120,910 kutoka kwa sampuli 1,414,865.

Katika visa hivi vipya, 710 ni raia wa Kenya huku 37 wakiwa raia wa kigeni, 396 ni wa kiume na 351 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi saba huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 114 wamepona virusi vya corona, 74 walipona wakiwa nyumbani huku 40 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 89,508 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 17 waliaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 2,011 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 889 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 2,545 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 121 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)