Hakutakuwa na sherehe za Pasaka katika makanisa ya Nairobi, Nakuru - Baraza la dini

Archbishop Anthony Muheria picha : The-star.co.ke
Archbishop Anthony Muheria picha : The-star.co.ke

Likizo za Pasaka ziko katika hali isiyojulikana kufuatia maagizo ya rais yanazuia sherehe hizo katika kaunti tano.

Shughuli za kuhudhuria ibada katika kaunti za Nairobi, Kiambu, Kajiado, Machakos na Nakuru kuabudu kibinafsi zilisimamishwa hadi hapo itakapotangazwa tena juu ya kuongezeka kwa virusi.

Hapo awali, wakristo wangesherehekea kila siku ya pasaka na pia kuhudhuria kesha.

Kila msimu wa sikukuu wakenya hurundikana kwenye mabasi yaliyojaa ili kurudi kwenye familia zao katika maeneo ya mashambani.

Baraza la uongozi wa dini linayoongozwa na Anthony Muheria katika taarifa Jumamosi lilithibitisha maagizo ya rais likisema kwamba yataathiri sherehe za Pasaka.

"Maagizo haya yatatumika hata kwa sherehe takatifu za Pasaka, Ramadhan na sikukuu za Wahindu ambazo zitakuwa katika kipindi hiki cha vizuizi," Muheria alisema.

"Kwa hivyo, katika maeneo ambayo kizuizi kamili kimewekwa, tutaabudu kupitia ibada ya mtandaoni," alisema.