Kwa wiki tatu nimekuwa hali mahututi kwa ajili ya corona-Raila asema

Muhtasari
  • Hatimaye nimetoka! Kiongozi wa chama cha ODM Raila amesema huku akieleza  jinsi aipambana na virusi vya corona baada ya kupatikana navyo mwei wa machi
  • Akizungumza wakati alipokagua miradi jijini Nairobi akiwa na rais, Raila alimshukuru Mungu kwa kumponya

Hatimaye nimetoka! Kiongozi wa chama cha ODM Raila amesema huku akieleza  jinsi aipambana na virusi vya corona baada ya kupatikana navyo mwei wa machi.

Akizungumza wakati alipokagua miradi jijini Nairobi akiwa na rais, Raila alimshukuru Mungu kwa kumponya.

"Wakenya wenzangu, niko nje! Mungu ni mwema. Leo, nimepata nafasi ya kuondoka nyumbani kwangu tangu nilipopatikana  na Covid-19," alisema kwa sauti ya kuchomoza.

Akiwa amesimama bega kwa bega na Rais Uhuru Kenyatta, Raila alisema ugonjwa huo ulimwacha mgonjwa mahututi.

"Kwa wiki tatu zilizopita, nilikuwa katika hali mbaya. Rais aliniita hapa ili niweze kukagua miradi pamoja naye,

Asante Uhuru kwa kunialika nitoke nje, ili Wakenya waweze kuona uso wangu. Nimefurahi kuona maendeleo katika kituo cha Green Park." Aliongea Raila.

Kigogo huyo alipopimwa tena siku ya jumatano hakupatikana na virusi hivyo.