ODM chasema Raila sio miongoni mwa wagombeaji wake

Muhtasari
  • Chama cha ODM cha weka wazi Raila sio miongoni mwa wagombea urais
  • Kupitia kwenye ukurasa wa chama hicho wa twitter alisema kwamba walipokea maombi ya viongozi wawili
b6251efb2cdb00bc
b6251efb2cdb00bc

Katibu Mkuu wa chama cha ODM, Edwin Sifuna amesema kuwa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga si miongoni mwa wagombeaji waliowasilisha maombi yao ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho mwaka 2022.

Kupitia kwenye ukurasa wa chama hicho wa twitter alisema kwamba walipokea maombi ya viongozi wawili.

"Mwisho wa kipindi , chama kilipokea Maombi mawili tu kutoka kwa Mheshimiwa Wycliffe Ambetsa Oparanya na Mheshimiwa Ali Hassan Joho, ”alisema Sifuna.

Alibainisha kuwa Waziri Mkuu wa zamani hakuomba tikiti ya chama kwa sababu ya msimamo wake wa muda mrefu kwamba hatajadili mambo ya 2022 hadi baada ya mchakato wa (BBI) kukamilika.

"Siasa ni biashara,na ni biashara ya kutiliwa maanani kila siku ya kalenda, wacha tarehe 1 Aprili ambapo tulijiunga na watu siku hiyo ya kudanganya

kupitia mawasiliano yetu tukijua marafiki zetu kwenye vyombo vya habari na siasa hawatajua vyema

Huu ndio msimamo,Raila Odinga hakutuma ombi la tikiti ya chama cha ODM, msimamo wake wa muda mrefu ni kwamba hatajadili mambo au siasa za mwaka wa 2022 hadi baada ya mchakato wa BBI utakapokamilika,"