Covid-19: watu 991 wapatikana na corona,370 wapona, 26 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 991 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 6,417 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Katika visa hivi vipya, 956 ni raia wa Kenya huku 35 wakiwa raia wa kigeni, 543 ni wa kiume na 448 ni wanawake

Kenya imerekodi visa 991 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 6,417 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 147,147 kutoka kwa sampuli 1,571,244.

Katika visa hivi vipya, 956 ni raia wa Kenya huku 35 wakiwa raia wa kigeni, 543 ni wa kiume na 448 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 7 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 99.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 370wamepona virusi vya corona, 214 walipona wakiwa nyumbani huku 156 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 99,580ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu  26 dunia kutokana na maambukizi kufikisha 2,394 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,607 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 5,996 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 293 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)