Covid-19: Watu 241 wapatikana na corona,20 waaga dunia

Muhtasari
  • Kati ya aambukizi hayo mapya 228 ni wakenya huku 13 wakiwa ni raia wa kigeni
  • Watu 636 wamepona maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 102,278 watu waliopona corona
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Watu 241 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 151,894 ya watu waliopatikana na corona ,hii ni kutokana na sampuli 2,515 zilizopimwa chini ya saa 24.

Kati ya Maambukizi hayo mapya 228 ni wakenya huku 13 wakiwa ni raia wa kigeni.

Pia 135 ni wanaume huku 106 wakiwa ni wanawake, mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 7  huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 90.

Watu 636 wamepona maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 102,278 watu waliopona corona.

Vile vile watu 20 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 2,501 ya watu walioga dunia kutokana na corona.

Wagonjwa 1,651 wamelazwa hospitali tofauti humu nchini huku 6,161 wakipokea matibabu wakiwa wamejitenga nyumbani.

Wagonjwa 250 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).