Chama cha Wiper chajiondoa NASA na kujiunga rasmi ni chama cha OKA

Muhtasari
  • Chama cha Democratic cha Wiper Jumatatu, Julai 26 kilitangaza kujiondoa kutoka kwa Muungano wa National Super Alliance (NASA)
Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka
Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka
Image: MERCY MUMO

Chama cha Democratic cha Wiper Jumatatu, Julai 26 kilitangaza kujiondoa kutoka kwa Muungano wa National Super Alliance (NASA).

Akiongea na wanahabari katika makao makuu ya Chama cha Wiper huko Karen, kiongozi wa chama Kalonzo Musyoka alisema kuwa chama hicho kilifanya uamuzi baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Kalonzo alifichua kwamba chama chake sasa kitazingatia juhudi zake kwa One Kenya Alliance  (OKA).

Alisema pia kwamba Wiper ilikuwa akifanya kazi kwa kushirikiana na Jubilee.

Makamu wa Rais wa zamani pia alikaribisha Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kujiunga na umoja huo. Alifuchua pia mipango ya kuzindua kampeni Jumanne.