Raila asafiri Zambia kwa hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya Hakainde Hichilema

Muhtasari
  • Raila asafiri Zambia kwa hafla ya kuapishwa kwa Rais mpya Hakainde Hichilema
Image: Raila Odinga/Twitter

Kinara wa ODM Raila Odinga amesafiri Zambia kwa ajili ya hafla ya  kuapishwa kwa rais aliyechaguliwa  Hakainde Hichilema.

Hichilema, ambaye alikuwa kiongozi wa Upinzani wa Zambia alimshinda Edgar Lungu baada ya kupata kura zaidi ya milioni 2.8 kwenye jaribio lake la sita.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter jioni ya Jumatatu, Agosti 23, kiongozi huyo wa ODM alitangaza kuwa amewasili katika taifa hilokwa ajili ya kuapishwa kwa Hichilema shughuli itakayofanyika Jumanne, Agosti 24.

"Nimewasili Lusaka, Zambia kwa hafla ya kuapishwa kesho kwa Rais Mteule Hakainde Hichilema. Itakuwa siku nzuri kwa watu wa Zambia na Afrika kwa jumla kushuhudia uhamishaji wa mamlaka bila mgogoro kama inavyotakiwa na michakato ya kidemokrasia," alisema.