Kilio cha haki!Seneta wa Lamu alimlazimisha Joy Makena kuchukua Ksh 70,000 baada ya kumpiga risasi

Muhtasari
  • Kulingana na Makena, Seneta huyo alimshurutisha kukubali suluhu la KSh 70,000 nje ya mahakama

Joy Makena, mwanamke aliyedaiwa kupigwa risasi na Seneta wa Lamu Anwar Loitiptip alilazimika kufanyasuluhu nje ya mahakama.

Kulingana na Makena, Seneta huyo alimshurutisha kukubali suluhu la KSh 70,000 nje ya mahakama.

Kwa upande wake, Seneta Anwar ataondoa kesi aliyokuwa amewasilisha dhidi ya marafiki wawili wa Makena waliokuwa naye usikuya kisa hicho.

“Anatishia wengine ambao hawakupigwa risasi anasema nikikataa hizo pesa wawili hao watafungwa jela.

Kwa hivyo, ikiwa ni wewe, ungefikiria kukubali, mtu maskini hana haki. Baba yangu alikuwa akiniambia nimsamehe kwa sababu tayari mimi ni mlemavu,” Joy Makena alisema.

Sasa, mwathiriwa anataka mamlaka husika kuingilia kati kesi hiyo na kumsaidia kupata haki.

"Sasa mimi ni mlemavu na watu wengi wananitegemea. Hivyo nikipata msaada katika kesi hii niko tayari kwenda naye mahakamani," aliomba.

Katika hati za kisheria ambazo Makena alilazimishwa kutia saini, pande zote mbili zilikubali kuondoa kesi hiyo kwa sharti kwamba Seneta Anwar Loitiptip atalipa bili za matibabu za Makena.

"Pande zote mbili baada ya utekelezaji wake zitaondoa malalamiko yaliyotolewa katika kituo cha Polisi cha Nanyuki kuhusu tukio la tarehe 24 Oktoba 2021.

"Hakuna upande utakaokuwa na madai yoyote dhidi ya mwingine juu ya matukio ya tarehe 24 Oktoba 2021 baada ya kutekelezwa," hati za suluhu, zilizochorwa na Chweya and Associates Advocates, zilisomwa kwa sehemu.