Nimechukizwa!Matiang'i ataka waendesha Boda Boda wakamatwe kwa kumshambulia mwanamke

Muhtasari
  • Akisema "ameshtuka na kuchukizwa", Dkt. Matiang'i alielekeza maafisa wa usalama kuwasaka watu hao waovu na kuona wanaadhibiwa kwa vitendo vyao viovu
Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiang'i
Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiang'i
Image: Picha:HISANI

Waziri wa Usalama wa Ndani ametoa agizola tukio  ambapo dereva wa kike alivamiwa na genge la waendesha boda boda

Akisema "ameshtuka na kuchukizwa", Dkt. Matiang'i alielekeza maafisa wa usalama kuwasaka watu hao waovu na kuona wanaadhibiwa kwa vitendo vyao viovu.

"Nimeshtushwa na kuchukizwa na video iliyosambaa ya mwendesha gari wa kike akinyanyaswa na washukiwa waendesha bodaboda kwenye barabara ya Wangari Maathai/Forest. Ni lazima tulinde barabara zetu dhidi ya vitendo hivyo viovu na vya kukemea," alisema katika taarifa yake iliyotolewa. kwenye mitandao yake ya kijamii.

Aliendelea na kusema;

"Nimewaomba maajenti wetu wa usalama kuhakikisha kwamba wahusika wote wa kitendo hiki kiovu wanakamatwa haraka na kuadhibiwa ipasavyo kwa kitendo chao hicho kiovu."

Huduma ya Polisi ya Kenya ilisema wanaifahamu video hiyo na kuiita "ya kuchukiza", polisi, katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao yao ya kijamii, walisema walitambua baadhi ya watu hao na wanawawinda.