Mtahiniwa wa KCSE azirai na kuaga dunia wakati wa mtihani

Muhtasari
  • Mtahiniwa wa KCSE azirai na kuaga dunia wakati wa mtihani
May-You-Rest-In-Peace-quotes-images-pictures-download-1
May-You-Rest-In-Peace-quotes-images-pictures-download-1

Hali ya huzuni ilitanda katika Shule ya Upili ya Chilchila huko Kipkelion, Kaunti ya Kericho baada ya mtahiniwa kuzimia na kufariki mara baada ya kuanza kuandika karatasi yake ya mtihani wa KCSE.

Kamishna wa Kaunti ya Kericho Kamau Karungo alithibitisha kisa hicho akisema mtahiniwa huyo alianguka katika chumba cha mtihani alipokuwa akikaribia kuanza kuandika karatasi yake ya Kiingereza.

Karungo alisema mtahiniwa huyo alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Fort-Tenan ambako alitangazwa kuwa amefariki alipofika.

Alisema chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika kwani mtahiniwa alikuwa mzima kabla ya kuanza kwa mtihani na amekuwa mzima kwa muda wote.

Kulingana na wahudumu wa hospitali hiyo ambao hawakutaka kutajwa majina, wazazi wa mtahiniwa huyo waliripoti kwamba amekuwa na afya njema muda wote na hakuwa ameonyesha dalili zozote za ugonjwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Huduma kwa Walimu Nancy Macharia alidokeza kuwa walimu 70,486 walikuwa wamekaguliwa kwa kina ili kusimamia mitihani ya kitaifa.

Wizara ya Elimu ilifichua kuwa watahiniwa 831,015 watafanya mitihani ya KCSE ya 2021 iliyoanza Jumatatu asubuhi, Machi 14 na kuendelea hadi Ijumaa, Aprili 1.