Mwalimu mjamzito abakwa na genge la majambazi

Mwalimu huyo kwa sasa yuko hospitali ya kaunti hiyo.

Muhtasari

•Mwalimu mkuu wa shule aliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Kainuk siku ya Jumatatu.

Maafisa wa polisi wakipiga doria
Image: bbc

Mwalimu mjamzito katika shule moja kwenye mpaka wa Kaunti za Turkana na Pokot Magharibi nchini Kenya alibakwa Jumapili usiku na genge la majambazi waliojihami ambao kwa sasa wanawawanyasa wakaazi na maafisa wa usalama huko Kainuk.

Mwalimu mkuu wa shule aliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Kainuk siku ya Jumatatu.

Mwalimu huyo alibakwa na majambazi wanne ambao walitishia kumuua yeyote ambaye angepiga kelele, kulingana na mwalimu mkuu.

"Mwalimu alikuwa aanze likizo yake ya uzazi mwezi ujao. Walimu watano waliobaki shuleni wametishia kujiuzulu kwani maisha yao yako hatarini. Wanafunzi hawajaripoti shuleni leo," mkuu wa shule alisema kituoni hapo.

Mwalimu huyo kwa sasa yuko hospitali ya kaunti hiyo.