Kanisa lafungwa kwa kufundisha waumini kutoenda hospitalini, kupelekea vifo vya watoto 4

Watoto 4 wagonjwa wameokolewa na kuwapelekwa hospitalini ambapo walibainika kuuguan nimonia na utapiamlo.

Muhtasari

•Kanisa la Naivasha limefungwa kutokana na madai ya vifo vya watoto 4 ambao wazazi walikosa kuwapeleka hospitalini kutokana na imani zao za kidini.

•DCC alisema waumini wa kanisa hilo waliokamatwa watashtakiwa katika mahakama ya Naivasha kwa kupuuza majukumu yao ya uzazi.

Waumini watatu wa dhehebu la 'Church of God' kutoka Maella, Naivasha wamekamatwa kwa madai ya kupuuza majukumu yao baada ya kukataa kuwapeleka watoto wao kwa huduma za matibabu kwa madai ya imani zao za kidini.
Waumini watatu wa dhehebu la 'Church of God' kutoka Waumini watatu wa dhehebu la 'Church of God' kutoka Maella, Naivasha wamekamatwa kwa madai ya kupuuza majukumu yao baada ya kukataa kuwapeleka watoto wao kwa huduma za matibabu kwa madai ya imani zao za kidini.
Image: ERASTUS GICHOHI

Mamlaka ya serikali mjini Naivasha imeamuru kufungwa kwa kanisa lenye utata kutokana na madai ya vifo vya watoto wanne kutokana na wazazi kukosa kuwapeleka hospitalini kutokana na imani zao za kidini.

Kanisa linalojulikana kama "Church of God" katika eneo la Maella mjini Naivasha lilikuja kuangaziwa baada ya waumini wake watatu kukamatwa kufuatia malalamiko ya umma baada ya kukataa kuwapeleka watoto wao waliokuwa wagonjwa hospitalini kwa madai ya imani zao za madhehebu.

Mwaka huu pekee, watoto wanne wanadaiwa kufariki dunia kutokana na kutelekezwa na wazazi wao baada ya kujisikia vibaya na baadaye kufariki dunia huku watatu kati yao wakiripotiwa kuzikwa katika viwanja vya kanisa hilo.

Sasa, Naibu Kamishna wa Naivasha Mutua Kisilu ameagiza kanisa hilo kufunga milango yake hadi polisi watakapokamilisha uchunguzi wao kuhusu madai ya kifo na kutotimiza wajibu wa wazazi.

Kisilu alisema polisi wamezindua msako mkali wa kumtafuta mchungaji wa kanisa hilo ambaye amekimbia eneo hilo baada ya wananchi kutaka akamatwe kufuatia tuhuma za kuwafunza waumini wa dhidi ya kutafuta huduma za afya.

Aliongeza kuwa polisi na wananchi tayari wamewaokoa watoto wanne waliokuwa wakiugua na kuwapeleka katika hospitali ya jirani baada ya kuugua kutokana na nimonia na utapiamlo.

"Tunamsaka kiongozi wa kanisa ambaye ametoroka eneo hilo baada ya maelezo kuibuka kuwa baadhi ya watoto waliokufa walizikwa katika eneo la kanisa katika hali isiyoeleweka", ilisema DCC.

DCC alisema waumini wa kanisa hilo waliokamatwa watashtakiwa katika mahakama ya Naivasha kwa kupuuza majukumu yao ya uzazi na kwa kukosa kuwapeleka watoto wao hospitalini.

Kanisa hilo ambalo lilifungua shughuli zake mwaka 2016 likiwa na waumini wanne pekee tangu wakati huo limeongezeka na kufikia waumini 26 likiwa na wito wa kudhibiti shughuli za kanisa ili kuzuia mafundisho zaidi ambayo yamewazuia waumini kutafuta huduma za afya.