Ababu kusukuma maudhui na filamu za Kenya duniani kote

Alitarajiwa kukutana na wadau mbalimbali na wawekezaji watarajiwa.

Muhtasari

• Hii itawezesha wasanii kutoka Africa kuteuliwa katika tuzo hizi.

Ababu Namwamba, Elsa Majimbo na Wengine

 Ababu Namwamba anajaribu kukuza maudhui na filamu za kenya dunani kote alipotembelea Los Angeles, California na kukutana na mwanzilishi wa 1500 sound Academy Larrance Dopson. Walichunguza fursa za ushirikiano na kuwafunza wasanii ambao wako katika programu ya Talanta Hela.

Alikutana na mkubwa wa Invention Studios, bwana Nicholas Weinstock. Alitaka kuendeleza maendeleo ya makubaliano iliyosainiwa mwaka jana ambapo nyumba ya kutengeneza filamu walijitolea kutengeneza filamu 15 pamoja na kutoa ujuzi ya maendeleo ya uwezo kwa waundaji wa maudhui Kenya. 

Mktaba huu ulikua unaenda kufungulia wana filamu wa Kenya njia ya kuweza kushirikiana na  Invention Studios na kutengeneza filamu ambazo zitatambulika duniani kote.

Alikutana pia na  mkurugenzi mtendaji wa recording studio bwana Panos A. Panay na mkurugenzi mtendaji wa  Rwanda Development Board Deputy Nelly Mukazayire kuongelelea masuala ya Grammys Africa Award.  Hii itawezesha wasanii kutoka Africa kuteuliwa katika tuzo hizi.

Ababu Namwamba alihudhuria pia tuzo la Grammy ambayo ilifanyika Februari 5 .Alipokelewa na mbalozi wa Los Angeles kwa Kenya Amb. Thomas Kwaka.Aliongozana na mkurugenzi mtendaji wa Kenya Film Commission, Bwana Timothy Owase.

Alikuwa na upendeleo wa kukutana na  Elsa Majimbo ambaye ni muundaji wa maudhui  na kumpa zawadi ya majani chai, maasai shuka na begi ya talanta Hela.

"You are an angel, Our tea. I have been drinking this tea for 22 years.  Blanket, tea and coffee in this cold weather. And I look like a proper Kenyan too". 

Larrance Dopson  katika mpini wake wa instagram aliandika " It's Time to shift Culture in Africa" ikisindikizwa na picha walipiga na Katibu wa baraza la mawaziri Ababu Namwamba na wengine.