Food 4 Education yapokea tuzo kubwa Miami, Florida

Wawira Njiru ametambuliwa kama mshindi wa wa Elevate Prize mwaka

Muhtasari
  • Alipokea taarifa ilo na kuichapisha kwa mtandao wake wa Instagram akijulisha wanaomfuta habari hiyo. Uso wake pia uliwekwa katika "The Time Square Manhattan, New York."
  • Shirika ya Food 4 Education ilianzishwa Januari 9, 2012 wakati bado alikuwa anafanya shahada yake ya lishe huko chuo kikuu cha South Australia.
Wawira Njiru
Image: Instagram

Mjasirimali, mwanzishi na mkurugenzi mtendaji wa Food for Education Wawira Njiru ametambuliwa kama mshindi wa  Elevate Prize mwaka huu kando ya viongozi wengine tajika.

Alipokea taarifa hiyo na kuichapisha kwa mtandao wake wa Instagram akijulisha wanaomfuata habari hiyo. Picha yake pia iliwekwa katika "The Time Square Manhattan, New York."

"Nimefurahi na kushukuru kutajwa kuwa mmoja wa washindi wa tuzo bora za mwaka huu pamoja na viongozi wengine wanaofanya kazi ya ajabu duniani. Pia kuwa kwenye Time Square. Ahadi yetu katika Elimu ya Food 4 ili kumaliza njaa darasani ndiyo maana tunaweka #KulishaWakati ujao. Hakuna mtoto anayepaswa kujifunza akiwa na njaa. Sasa tunalisha zaidi ya watoto 300,000 kote nchini Kenya".

Shirika ya Food 4 Education lilianzishwa Januari 9, 2012 wakati bado alikuwa anafanya shahada yake ya lishe huko chuo kikuu cha South Australia.

Food 4 Education huwezesha watoto walio katika hali ya hatarini kusoma kama wameshiba. Kupitia majukwa yao ya rununu Tap to Eat, wazazi hao wanalipia chakula ya watoto wao kwa bei nafuu kwa kutumia malipo ya simu.

Wawira Njiru
Image: Instagram

Miaka 12 iliyopita, F4E ilipika chakula yake ya kwanza kwa watoto 12 lakini sai wameongeza watoto 100,000 kwa programu yao.

Baadhi ya mafanikio yake ni;

2017- Mpokeaji mdogo wa chuo kikuu cha South Australian's Alumni Awards. 

2018- Mpokeaji wa kwanza wa tuzo la Global Citizen Youth Leadership Prize iliyotolewa na Cisco.

2020- Ford Foundation Global Fellow.

2021- UN Kenya Person Of The Year, World Economics Forum Young Global Leader Class.

2023- Tuzo La Pulse Influencers; Positive Impact Influencer Of The Year.

2024- Elevate Prize