Bosi wa Cotu, Francis Atwoli amuaga mlinzi wake mwaminifu akistaafu baada ya miaka 20

Katibu Mkuu wa Cotu Francis Atwoli amemuaga afisa wake wa usalama Sergent Robert Chembe.

Muhtasari

•Bosi huyo wa Cotu alisema Chembe amekuwa afisa wake wa usalama kwa miaka 20 na ataenda kwa likizo akisubiri kustaafu.

•Katika taarifa yake Jumamosi, Atwoli alimtaja kama mtu mwaminifu na wa kuaminika.

Atwoli amemuaga afisa wake mwaminifu wa usalama anapostaafu baada ya miaka 20
Atwoli amemuaga afisa wake mwaminifu wa usalama anapostaafu baada ya miaka 20
Image: HISANI

Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (Cotu) Francis Atwoli amemuaga afisa wake wa usalama Sergent Robert Chembe.

Katika taarifa yake Jumamosi, Atwoli alimtaja kama mtu mwaminifu na wa kuaminika.

Bosi huyo wa Cotu alisema Chembe amekuwa afisa wake wa usalama kwa miaka 20 na ataenda kwa likizo akisubiri kustaafu.

"Ninamuaga afisa wangu mwaminifu na wa kuaminika wa usalama Sergent Robert Chembe, ambaye amekuwa nami kwa zaidi ya miaka ishirini. Sasa anaendelea na likizo akisubiri kustaafu, Mungu ambariki Yeye na Familia Yake," Atwoli alisema.

Atwoli ni mwanaharakati mkongwe wa vyama vya wafanyakazi ambaye ametumikia Cotu kwa miaka mingi.

Bosi huyo wa Cotu pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mashamba na Kilimo Kenya (KPAWU) na hivi majuzi alichaguliwa tena kuwa Rais wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi barani Afrika (OATUU).

Alichaguliwa kuhudumu katika nafasi hiyo kwa muhula wa tatu mfululizo.

Uchaguzi ulifanyika Novemba 2023, wakati wa Kongamano la 12 la OATUU mjini Algiers, Algeria.

OATUU iliyoanzishwa mwaka wa 1973 na yenye makao yake makuu jijini Accra Ghana, ndiyo shirika pekee la vyama vya wafanyakazi barani Afrika ambalo linawakilisha maslahi yote ya vyama vya wafanyakazi barani Afrika.

Atwoli pia hutumikia wafanyikazi kama mwanachama anayejulikana wa Shirika la Uongozi la Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Wafanyakazi.