Madai ya Swaleh Mdoe kusimamishwa kazi yazua mjadala mitandaoni

Mwanahabari wa runinga wa citizen amesimamishwa kazi kwa kuwa alikosa taarifa moja.

Muhtasari
  • Mwanahabari wa runinga wa citizen amesimamishwa kazi kwa kuwa alikosa taarifa moja. Inasemekana kuwa jumanne, Januari 23 alienda kupokea matibabu siku hiyo na hakuelezea msimamizi wake. 
Swaleh Mdoe

Madai kuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Swale Mdoe amesimamishwa kazi yamezua mjadala mitandaoni.

Inasemekana kuwa Mdoe alichukuliwa hatua baada ya kukosa kufika kazini kusoma taarifa. 

Inadaiwa kuwa jumanne, Januari 23 alienda kupokea matibabu siku hiyo na hakufahamisha msimamizi wake. 

Uamuzi wake wa kukosa kukuja kazi bila kuambia msimammizi wake ulifanya mkurugenzi wa uhariri kuamua kumsmamisha kazi. Aliitwa na wakubwa wake na kuelezewa kuhusu uamuzi huo.

Tangu usimamishi  wake, Mdoe bado alikuwa anaenda kazini kama kawaida.

Mdoe alikuwa anasoma habari ya Prime-Times swahili Jumatatu saa moja usiku na taarifa ya saa saba, Jumanne, Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.

Mdoe ni mwandishi wa habari na mhariri mkuu Royal Media Services.

Mwanahabari huyo alianza kazi yake mwaka wa 1999 Nation Media hadi 2001 baada ya hapo alienda runinga ya KTN kuanzia 2001-2007. Hapo alikuwa mhariri habari na pia mtangazaji wa habari.

Kuanzia mwaka wa 2007 amekuwa mhariri mkuu na mwanahabari wa kiswahili Roya Media ( Runinga ya Citizen). Amekuwa runinga ya Citizen kwa miaka 17.