Jaji mkuu Martha Koome aomboleza jaji mstaafu Akiwumi

Safari ya Akiwami katika sekta ya haki ilitiwa alama kwa utumishi wake akiwa hakimu wa mahakama kuu ya Kenya

Muhtasari
  • kupitia huduma yake, Akiwami pia aliteteanchi na jamii imara nanga katika utawala wa sheria na utulivu wa kikatiba.
  • Aliongeza kuwa alikuwa mwema, mkarimu, jasiri na mwenye busara na aliathiri maisha ya watu wengi.
Jaji Mkuu Martha Koome
Image: BBC

Familia ya mahakama akiongozwa na jaji mkuu Martha Koome, wameomboleza marehemu jaji Akilano Molade Akiwumi.

Safari ya Akiwami katika sekta ya haki ilitiwa alama kwa utumishi wake akiwa hakimu wa mahakama kuu ya Kenya kuanzia mwaka wa 1987 hadi 1993 na baada ya hapo alikuwa jaji wa mahakama ya rufaa kuanzia 1993 hadi 2001.

Alistaafu baada ya muda wake katika mahakama ya rufaa.

Pia aliwahi kuwa jaji na rais wa Comesa court of Justice kuanzia mwaka wa 2000 hadi 2003, ambapo alishinda kuvuka mpaka ushirikiano wa mahakama na kulinganisha maendeleo ya pamoja.

Kwa ujumbe wa rambirambi iliyoandikwa na Koome, alisema kuwa marehemu jaji Akiwumi, alikuwa mzalendo ambaye bila kuchoka alitumikia nchi yetu kama jaii anayeheshimika.

"He was known for enriching our legal framework and also significantly contributed to its development,"  Jaji mkuu alieleza.

kupitia huduma yake, Akiwami pia aliteteanchi na jamii imara nanga katika utawala wa sheria na utulivu wa kikatiba.

Aliongoza Tume ya uchunguzi ya Akiwami  katika mapigano ya kikabila ambayo ambayo iliteuliwa mwaka wa 1998 kuchunguza makabila mbalimbali katika nchi.

Kufuatia kustaafu kwake kama jaji, alikuwa wakili mkuu kwa Alternative Dispute Resolution (ADR), kuwa msuluhishi Katika migogoro mingi ya kibiashara.

Koome alibainisha kuwa kazi ya Akiwami ya kutambulisha ADR, Imesababisha matumizi yake kama taratibu ya kutatua migogoro.

"His work was the foundation of past, present and future endeavours to anchor values of inclusivity and cohesion in our beloved nation", Koome alisema.

Mbali na kuwa mfanyakazi mzuri, jaji mkuu Koome alimueleza kama, "Mentor and friend to many within the judiciary and the broader legal fraternity".

Aliongeza kuwa alikuwa mwema, mkarimu, jasiri na mwenye busara na aliathiri maisha ya watu wengi.

"May the memories of justice Akiwami's remarkable life and enduring contributions to justice provide solace to us all the inspiration to present and future generations of legal practitioners," Koome alisema.