Maswali yameibuka kuhusu wabunge ambao hawakujitokeza kupiga kura ya makazi ya gharama nafuu

UDA walijitokeza kwa wingi kusaidia mradi wake President William Ruto.

Muhtasari
  • Baadhi ya wabunge ambao hawakuwa ni  Babu Owino ( Embakasi East), Peter Salasya ( Mumias East) , Naisulu Lesuuda (Samburu East), Timothy Wanyonyi (Westlands), Beatrice Elachi na (Dagoretti North) .
Bunge la Kenya
Bunge la Kenya
Image: Twitter @NAssembly Kenya

Wakati wa shauri hilo, wabunge walishirikiana na chama cha UDA walijitokeza kwa wingi kusaidia mradi wake President William Ruto. 

Wakati kura ilikuaikiendelea, wakenya walitazama kwa makini kuwa kuna wabunge wa chama cha Azimio ambao hawakuwepo.

Baadhi ya wabunge ambao hawakuwa ni  Babu Owino ( Embakasi East), Peter Salasya ( Mumias East) , Naisulu Lesuuda (Samburu East), Timothy Wanyonyi (Westlands), Beatrice Elachi na (Dagoretti North) .

Babu Owino huku akieleza kutokuwepo kwake, alishiriki picha zake akifundisha darasa la hisabati county ya Kisumu katika mtandao wake wa kijamii.

Mwakilishi wa wanawake wa nairobi Esther Passaris ambaye ako katika chama cha ODM,  pia hakuwepo.

Kwa wakati huo maalum alikuwa akihudhuria warsha ya kuzingatia jinsia kwa wabunge wanawake.

Kwa upande mwingine, mbunge wa Githunguri Gathoni Wamuchomba ambaye licha ya kuchaguliwa kwa tiketi cha UDA, pia hakuwepo wakati kura ulikuwa unapigia.

Kabla ya kura kupigwa, kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kimani Ichung'wah, alitoa wito kwa wabunge wenzake kuzingatia washirika wao wakati watapiga kura.

" Vote for jobs!jobs! Vote for wealth creation and vote for a nnew Kenya", Ichung'wah alieleza