Mwanamke afika mahakamani kusimamisha mazishi ya Kiptumu kwa sababu anadai kuwa na mtoto wake

Anadai kuwa wako na mtoto ambaye ako mwaka mmoja miezi 7 ambaye haki zake zinaweza kukiukwa ikiwa mazishi hayatasimamishwa.

Muhtasari
  • Hakimu Wananda alikataa kusimamisha mazishi kutokana na madaiwa ya mwanamke huyo Edna Owuor kupitia wakili wake Joseph Oyaro.
Edna Awuor Atieno nje ya mahakama kuu ya Eldoret

Mahakama kuu ya Eldoret imekataa kusimamisha mazishi ya mwanariadha Kelvin Kiptum kufuatia madai ya mwanamke wa miaka 22 kukuwa na mtoto na mwanariadha huyo.

Hakimu Wananda alikataa kusimamisha mazishi kutokana na madaiwa ya mwanamke huyo Edna Owuor kupitia wakili wake Joseph Oyaro.

Anadai kuwa wako na mtoto ambaye ako mwaka mmoja miezi 7  ambaye haki zake zinaweza kukiukwa ikiwa mazishi hayatasimamishwa.

Wakili Owuor alionekana kotini na mtoto huyo kutaka kusimamisha mazishi ambayo ilikuwa imetangazwa kufanyika Februari 22 mwaka huu huku  akisema kuwa hawakumshirikisha mwanamke huyo katika mipango ya maziko.

Mwanamke huyo pia alitaka Sampuli za DNA zichukuliwe  kutoka kwa mwili ili kubaini kuwa Kiptum ndiye baba mtoto.

Hakimu Wananda alisema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa imeendelea kwa muda kwa gharama kubwa na itakuwa si haki kusitisha maziko.