Vivo Energy Imeanzisha kampeni ya Tu-sort Garage na Shell Lubricants

Ikiwa wewe ni mmiliki wa karakana au fundi, jiandikishe kwenye kampeni hii na uwaombe wateja wako kuteua na kuipendekeza gereji yako. Kampeni itaanza Machi 4 na kuendelea hadi Juni 2, 2024 kwa muda wa wiki 12.

Muhtasari

• Ili kusaidia makanika na wamiliki wa gereji, Shell imezindua kampeni ya Tu-sort Garage na Shell Lubricants.

Makanika na wamiliki wa karakana mara nyingi hutatizika kupata zana na vifaa vya hali ya juu vinavyohitajika kwa matumizi ya kipekee.

Zaidi ya hayo, kuenea kwa bidhaa bandia za mafuta ya kulainisha kumezidisha changamoto zao. Kwa kukabiliana na hili, Shell inatoa mafuta halisi ya kulainisha, ya hali ya juu ili kuhakikisha utendakazi bora wa gari na pia kukabili bidhaa ghushi.

Kwa mujibu wa ripoti ya toleo la 19 ya Kline & Company yenye mada, “Global Lubricants: Market Analysis and Assessment 2021,” mafuta ya kulainisha ya Shell yameshikilia nafasi ya juu ya chapa ulimwenguni kwa miaka 15 mfululizo.

Ili kusaidia makanika na wamiliki wa gereji, Shell imezindua kampeni ya Tu-sort Garage na Shell Lubricants. Ikiwa wewe ni mmiliki wa karakana au fundi, jiandikishe kwenye kampeni hii na uwaombe wateja wako kuteua na kuipendekeza gereji yako.

Ili karakana ifuzu katika promosheni hii, ni lazima:

 Iwe imesajiliwa kwa kampeni ya Tu-sort Garage na Shell Lubricants.

 Iwe na kibali halali cha kuhudumu kibiashara.

 Iwe inafanya kazi kutoka eneo halisi linalojulikana au eneo la biashara.

 Iwe inauza au kutumia bidhaa halisi za mafuta ya kualinisha ya Shell Lubricants.

Ili kuteua karakana, mshiriki anapaswa kufuata hatua hizi:

 Piga USSD 459*200# kutoka kwa simu yako (bila malipo).

 Chagua chaguo la 1 ili kuingiza nambari ya kodi

 Weka nambari ya kodi kutoka kwa kifuniko cheusi cha Shell Lubricant.

 Chagua chaguo la 2 kwa “TUSORT GARAGE na SHELL LUBRICANTS”

 Thibitisha makubaliano ya sheria na masharti.

 Chagua Chaguo 2 ili kuteua karakana.

 Weka nambari ya kodi ya karakana husika

Karakana tatu za kwanza zilizo na uteuzi mwingi wa kila mwezi zitapokea vifaa vya kitaalamu kama vile alama za nje za kibiashara, vionyesho vyenye chapa, sare za wafanyakazi, trei za kutolea mafuta, jaki, stendi za jeki, na visanduku vya kuweka vifaa. Karakana ya nchi nzima yenye uteuzi wa juu zaidi itakabidhiwa uboreshaji wa kipekee.

Kampeni itaanza Machi 4 na kuendelea hadi Juni 2, 2024 kwa muda wa wiki 12. Kwa maswali, wasiliana na mhudumu wa wateja wa Vivo Energy kupitia 0701119634, Jumatatu hadi Ijumaa, saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Shiriki katika promosheni hii, usifungiwe nje ya kuboresha huduma zako. Jisajili na uhamasishe wateja wako leo. Tu-sort Garage na Shell Lubricants - ambapo ubora unakidhi upekee wa huduma!