RIP! Kaka ya Gavana Lusaka afariki katika ajali ya barabarani

Marehemu alifariki papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga tela la miwa.

Muhtasari

•Alifariki katika ajali mbaya ya barabarani katika soko la Kamukunywa, kaunti ya  Bungoma mnamo Jumamosi usiku.

Marehemu Noah Lusaka
Image: HISANI

Noah Lusaka, nduguye Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka amefariki.

Alifariki katika ajali mbaya ya barabarani katika soko la Kamukunywa, kaunti ya  Bungoma mnamo Jumamosi usiku.

Marehemu alifariki papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga tela la miwa.

Mnamo Jumapili, Gavana Lusaka alitangaza kifo hicho katika taarifa kwenye mitandao yake ya kijamii.

"Rambirambi zangu za dhati ziende kwa mama yangu, ndugu, jamaa, marafiki na jamaa katika kipindi hiki kigumu sana," Gavana Lusaka alisema.

Gavana huyo alimtaja kaka yake kuwa mtu wa kipekee ambaye aliacha hisia za kudumu kwa kila mtu aliyekutana naye.

“Tunapohuzunika kwa msiba huu mzito, ninapata kitulizo kwa kuthamini kumbukumbu nzuri tulizoshiriki. Fadhili, kicheko, na upendo wa Noah vitakuwa sehemu yetu milele,” aliongeza.