'Alikasirika sana' Bintiye Lizzie Wanyoike afichua hisia za mamake baada ya kugunduliwa na saratani

Lizzie alifariki wiki iliyopita baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Muhtasari

•Licha ya kusafiri kwa hospitali tofauti, hakuna utambuzi wa ugonjwa uliofanywa katika miaka ya mapema ya ugonjwa wake.

•"Tulisafiri hadi India, Marekani tukitamani sana kujua ni nini kilikuwa kinamsumbua," bintiye Wanyoike alisema.

Marehemu Lizzie Wanyoike
Image: HISANI

Mwanzilishi wa NIBS Lizzie Wanyoike amezikwa leo, Januari 22.

Lizzie alifariki wiki iliyopita baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Habari za vita vyake na saratani ziliwekwa wazi baada ya kifo chake.

Binti yake Stella Wanjiru alisema Lizzie alianza kuugua miaka mitano iliyopita.

Licha ya kusafiri kwa hospitali tofauti, hakuna utambuzi wa ugonjwa uliofanywa katika miaka ya mapema ya ugonjwa wake.

"Kwa zaidi ya miaka mitano alikuwa hajisikii vizuri.

Lakini miaka mitatu iliyopita hali yake mbaya ilianza kuwa mbaya.

Kila alipokuwa akihudhuria mikutano ya shule, vikao vya bodi n.k. alikuwa mgonjwa ."

Stella aliongeza kuwa wakati huo walikuwa wamechanganyikiwa kwani madaktari hawakuweza kubaini ni nini kilikuwa tatizo la mama yao.

"Alitembelea madaktari wengi lakini hakuna kilichogunduliwa, hakuacha gharama ili kujua nini kilikuwa kinamsumbua.

Tulisafiri hadi India, Marekani tukitamani sana kujua ni nini kilikuwa kinamsumbua.

Tulikuwa tunafikiri kutojua ni mbaya zaidi kuliko kujua, hadi tukapata ukweli."

Lizzie alipokea vipi habari za ugonjwa huo?

"Hatua yake ya kwanza ilikuwa kwamba alikuwa na hasira sana. Hakuweza kuelewa jinsi wataalam walikosa kutambua ugonjwa huo mbaya sana."

Lakini alivaa silaha zake haraka akijiandaa kwa vita iliyokuwa mbele yake. Mwaka wa 2023 alipigana sana.

Tuliamini kweli atapona.

Saratani haikushinda, Mungu wetu amemchukua mama yetu nyumbani." Alimalizia